Home Uncategorized KUMBE, BEKI MANCHESTER UNITED ALIMPA HASIRA BILLY WA CHELSEA

KUMBE, BEKI MANCHESTER UNITED ALIMPA HASIRA BILLY WA CHELSEA



KIUNGO wa Chelsea, Billy Gilmour amesema aliweza kucheza vizuri katika mechi yao dhidi ya Liverpool baada ya kuamua kuwa imara kutokana na mkwara aliopigwa na beki wa Manchester United, Harry Maguire.

Gilmour mwenye umri wa miaka 18, amesema walipokutana na Man United alikuwa katika wakati mgumu kutokana na mkwara wa beki huyo pande la baba. 


“Ndio maana mechi dhidi ya Liverpool nilibadilika kabisa, niliona lazima niwe tofauti na nikafanikiwa kufanya vizuri. 

 “Wakati fulani Maguire alinikaba shingoni bila kosa, nilijua alitaka kunitoa mchezoni.”

Kwenye mchezo wa Kombe la FA England, Chelsea iliibamiza mabao 2-0 Liverpool na kuifungashia virago jumla huku wao wakitinga hatua ya robo fainali.

SOMA NA HII  SHIKHALO AFUNGUKIA ISHU YA KUWEKWA BENCHI NA MNATA