Home Uncategorized MILIONI 200 ZAWEKWA MEZANI KWA YANGA KUIUA SIMBA MACHI 8 TAIFA

MILIONI 200 ZAWEKWA MEZANI KWA YANGA KUIUA SIMBA MACHI 8 TAIFA



UONGOZI wa Yanga na mdhamini GSM wameahidi kutoa Sh milioni 200 kwa wachezaji wa Yanga iwapo watashinda mechi yao dhidi ya Simba Jumapili, Machi 8, kwenye Uwanja wa Taifa.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema wadhamini wa GSM wameweka mezani Sh200 Milioni kwa wachezaji endapo watapata ushindi wa aina yoyote siku hiyo. 


“Hata wakichukua ubingwa sio tatizo, tunachohitaji ni kuwachapa, nadhani raha ya ubingwa utakuwa umeisha na kuwanyamazisha kupiga kelele hovyo mtaani.

 “Tulikuwa na utaratibu wa kutoa motisha kila wanaposhinda kwenye michezo ya Ligi Kuu hupewa Sh 10Milioni, lakini kutokana na umuhimu wa mchezo wa Jumapili tumeamua kufanya kitu kwa wachezaji ili kuweka raha Jangwani,’ amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YAINGIA ANGA ZA NAHODHA WA BIASHARA UNITED