Home Habari za michezo BAADA YA KAUNZA LIGI KWA MOTO WA AINA YAKE…MAYELE ATAMBA KUZIDI KUWAKERA...

BAADA YA KAUNZA LIGI KWA MOTO WA AINA YAKE…MAYELE ATAMBA KUZIDI KUWAKERA KWA KUTETEMA…


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kuwa mambo mazuri yanakuja na wameanza msimu huu wa 2022/23 pale walipoishia msimu uliopita.

Nyota huyo ameanza kufungua kapu la magoli akiifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakati wakishinda mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Mayele alisema wamerejea katika ligi msimu huu kuendelea walipoishia msimu uliopita kwa sababu wanahitaji kutetea mataji yao yote baada ya kufanikiwa kutwaa Ngao wa Jamii.

Alisema walianza dhidi ya Simba kwa kutetea taji la Ngao ya Jamii, wakafuata Polisi Tanzania kwenye Ligi Kuu kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini jambo ambalo ni mwanzo mzuri kwao.

“Pointi tatu ugenini ni jambo zuri na nimeendelea kufunga, bao la kwanza sasa tunaendelea tulipoishia na tunawahakikishia mashabiki mambo mazuri yanakuja zaidi ya waliyopata msimu uliopita,” alisema Mayele.

Alisema kocha Nabi (Nasreddine) ameona mapungufu yao na kuyafanyia kazi ili kutorudia katika mchezo wao ujao dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kesho, Jumamosi.

SOMA NA HII  BIL 25 ZATENGWA KUMVUA YANGA UBINGWA WA NBC....MO DEWJI ATAJWA..ISHU NZIMA IKO HIVI....