Home Habari za michezo KIUNGO WA SIMBA AFUNGUKA MAKALI YA YANGA YA GAMONDI

KIUNGO WA SIMBA AFUNGUKA MAKALI YA YANGA YA GAMONDI

Habari za Yanga

KIUNGO wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Simba SC, Amri Kiemba, amesifu aina ya soka wanalocheza mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, huku akiwatahadharisha wapinzani wao.

Yanga imekuwa na mfululizo wa ushindi wa mabao mengi katika michezo mitatu mfululizo, ikiwemo miwili ya Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika waliyocheza Uwanja wa Azam Complex, Dar. Matokeo ya Ligi Kuu Bara yalikuwa hivi; Yanga 5-0 KMC na Yanga 5-0 JKT Tanzania, huku Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa Yanga 5-1 ASAS.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kiemba alisema Yanga wanaendelea kuonesha kile ambacho walikianza tangu msimu uliopita kwa kupata matokeo mazuri, sambamba na kutoa burudani kucheza soka safi na kuvutia.

Kiemba alisema kuwa, Yanga ya msimu huu imetuma ujumbe kwa timu zinakuja mbele yao, kama utacheza katika nusu yako, basi wanaanzia hukohuko kukushambulia, huku wakiwazuia makipa wao, Djigui Diarra na Metacha Mnata wasifikiwe kirahisi.

Aliongeza kuwa, amefuraishwa na aina ya soka la kushambulia linalochezwa na Yanga, huku wakitumia nafasi nyingi katika kufunga mabao kwa kuongeza idadi ya wachezaji ndani ya boksi la wapinzani.

โ€œKwa hiki ambacho kinaendelea kwa Yanga, ni mwendelezo wa kile ambacho wameanza nacho, msimu uliopita walikuwa wanatengeneza nafasi nyingi, lakini walikuwa hawazitumii vizuri katika kufunga mabao.

โ€œLakini msimu huu utaiona Yanga wakishambulia pamoja wakati wakiwa na mpira tena kwa spidi kubwa, huku wakicheza soka safi la pasi wakiwatumia viungo kutengeneza nafasi za kufunga mabao.

โ€œWakishambulia goli la wapinzani utawakuta wachezaji kuanzia wanne hadi watano, Yanga hii mpya imetuma ujumbe kwa timu zinazokuja mbele yao, kujiandaa kama utacheza kwenye nusu yako ukijilinda, basi wao wanaanzia hukohuko kukushambulia, hivyo kipa wao hafikiwi kabisa, โ€œ alisema Kiemba ambaye pia aliwahi kuzichezea Yanga na Azam FC.

SOMA NA HII  STAA YANGA:- MAYELE AKIACHA UCHOYO TUTASHINDA...USILAZIMISHE KUFUNGA TOA PASI