Home Burudani KISA MANDONGA KUPEWA MADILI YA PESA NA UMAARUFU…SHABANI KAONEKA ALIA…ADAI YEYE ALIYESHINDA...

KISA MANDONGA KUPEWA MADILI YA PESA NA UMAARUFU…SHABANI KAONEKA ALIA…ADAI YEYE ALIYESHINDA NI MASKINI…


Bondia wa ngumi nchini, Shabani Kaoneka amewalalamikia waandishi wa habari kuwa wanaegemea upande wa bondia Karim Mandonga na kumpa fursa mbalimbali licha ya kuwa yeye ndiye mshindi wa pambano.

“Yule amepata bahati kuliko mimi, kwa sababu hata nyie waandishi wa habari wakati mwingine mnakuwa wanafiki, mkimuona Kaoneka kaalikwa kwenye sehemu ndio mnasogea lakini mbona Mandonga mnamfanyia ‘suprise’ nyingi mnamuita twende sehemu hii na hii,?” amehoji Kaoneka.

Kaoneka ameongeza kuwa “mimi niliyeshinda nakuwa masikini, aliyepigwa anakuwa tajiri, mimi najisikiaje?

SOMA NA HII  WAKATI WAKIFUZU ROBO FAINAL KIBABE...MO DEWJI ALIPUKA NA JIPYA SIMBA..ADAI ANAPATA HASARA MNOO...