Home Habari za michezo PAMOJA NA YOTE ALIYOFANYIWA…ZORAN MAKI KAONA ISIWE KESI..KAAMUA KUWAACHI SIMBA UJUMBE HUU...

PAMOJA NA YOTE ALIYOFANYIWA…ZORAN MAKI KAONA ISIWE KESI..KAAMUA KUWAACHI SIMBA UJUMBE HUU MZITO…


Siku moja baada ya kuondoka Simba SC, Aliyekua Kocha Mkuu wa klabu hiyo Zoran Maki ametoa neno la shukurani kwa Viongozi, Wachezaji na Mashabiki.

Zoran aliondoka rasmi Simba SC jana Jumanne (Septemba 06), baada ya kuvunja mkataba wake kwa makubaliano na Viongozi wa Simba SC, na baadae ikathibitika amejiunga na Klabu ya Ittihad ya Misri.

Kocha huyo kutoka nchini Serbia ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa neno la shukurani kwa Simba SC, huku akionesha alifurahia uwepo wake ndani ya Simba SC kwa siku 56 tangu alipotangazwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari.

Zoran ameandika; “Napenda kuishuruku klabu hii kwa kunipa nafasi ya kipekee, asante kwa wote walioniamini na ninashukuru kwa kila kitu,”

Msimu huu pekee kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara aliyokiongoza kikosi hicho, Zoran ameshinda yote akianza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold Agosti 17 kisha ushindi wa 2-0 kutoka kwa Kagera Sugar Agosti 20 yote ikichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJOA...NI PATASHIKA NGUO KUCHANIKA KATI YA YANGA,SIMBA, AZAM NA GEITA...MAMBO LAZIMA YWE MAGUMU...