Home Habari za michezo PAMOJA NA KUTOPATA NAFASI YA KUCHEZA….NGUSHI AFANYIWA HILA YANGA…JINA LAKE LAKOSEKANA USAJILI...

PAMOJA NA KUTOPATA NAFASI YA KUCHEZA….NGUSHI AFANYIWA HILA YANGA…JINA LAKE LAKOSEKANA USAJILI WA CAF…

Mshambuliaji Crispin Ngushi hatoichezea Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya klabu hiyo kutosajili jina lake litumike katika mashindano hayo msimu huu.

Orodha iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikionyesha usajili wa Yanga kwa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, haina jina la Ngushi huku ikifafanua kuwa klabu yake haijamjumuisha.

“Mchezaji Crispin Ngushi hakupitishwa na CAF kutokana na Young Africans kushindwa kumfanyia usajili kwenye mfumo wa usajili wa ndani TFF/FIFA Connect,” imefafanua taarifa hiyo yenye orodha ya wachezaji wa Yanga waliosajiliwa

Kikosi hicho cha wachezaji 27 waliosajiliwa kinaundwa na makipa Abutwalib Mshery, Johora Erick na Djigui Diarra wakati mabeki ni Hamad Ibrahim,David Brayson,  Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Lomalisa Mutambara, Kibwana Shomari, Djuma Shaban na Abdallah Shaibu.

Viungo ni Zawadi Mauya, Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Salum Abubakar, Faridi Musa, Feisal Salum, Yannick Bangala, Aziz Ki na Ducapel Moloko wakati washambuliaji ni Yusuph Athuman, Fiston Mayele, Bernard Morrison, Lazarous Kambole, Denis Nkane, Heritier Makambo na Dickson Ambundo

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA