Home Uncategorized MBRAZILI WA SIMBA AJIPA JINA JIPYA, HILI HAPA

MBRAZILI WA SIMBA AJIPA JINA JIPYA, HILI HAPA

GERSON Fraga, nyota wa Simba ambaye ni raia wa Brazil amesema kuwa mtindo wake wa ushangiliaji ni jina lake jipya ambalo amepewa na mashabiki pamoja na wachezaji wenzake.
Fraga amehusika kwenye mabao matatu kati ya 63 yaliyofungwa na Simba kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo aliwafunga Coastal Union mabao mawili na KMC aliwatungua bao moja.
Akizungumza kuhusu mtindo wake wa kushangilia ambapo kila akifunga mabao alikuwa akionyesha mtindo wa mkasi kwa mikono alisema kuwa ni aina ya jina alilopewa ndani ya Simba.
“Nikifunga ninapishanisha mikono kwa spidi ikiwa inamaanisha kwamba mimi ni mkata umeme, namaanisha kwamba nimetoka kukata umeme,” amesema Fraga.
SOMA NA HII  2019/20 JUMLA YA MECHI 380 ZIMECHEZWA NA KUKUSANYA MABAO 767