Home Yanga SC HUU HAPA UKWELI KUHUSU ”MAHUSIANO YA KI…ZI..” KATI YA MANARA NA MWAMNYETO

HUU HAPA UKWELI KUHUSU ”MAHUSIANO YA KI…ZI..” KATI YA MANARA NA MWAMNYETO


MSEMAJI mpya wa klabu ya Yanga, Haji Manara amefichua siri yake na Bakari Mwamnyeto kwamba alikuwa na ndoto ya kufanya kazi na beki huyo.

Manara wakati anawatambulisha wachezaji wa Yanga amesema ; “Mwenyezi Mungu aliandika nije kufanya kazi na Nondo na ndoto imetimia,”

Kauli hiyo iliwafanya mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo kupiga shangwe wakati wa utambulisho huo na kunyamaza mpaka pale Mwamnyeto alipopanda jukwaani.

Ikumbukwe Mwanyeto alikuwa anatakiwa kusajiliwa na Simba lakini Yanga walimuwahi na kumsajili hali iliyowafanya mabosi wa Simba wamsajili pacha wake Ibrahim Ame.

SOMA NA HII  YANGA NOMA SANA YAWAPIGA PINI MASTAA WAKE WOTE....YACOUBA KUTUPIWA VIRAGO...