Home Yanga SC YANGA YAINGIA ANGA ZA BEKI MGHANA

YANGA YAINGIA ANGA ZA BEKI MGHANA


 IMEELEZWA kuwa beki wa kikosi cha Azam FC, Yakub Mohamed raia wa Ghana yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Yakub amekuwa hana nafasi kubwa msimu huu kuanza kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba ndani ya Azam FC jambo ambalo linatoa nafasi kwake kuweza kusepa ndani ya Azam FC.

Ugumu unakuja kwenye mkwanja ambao Yanga wanatakiwa kuutoa ili kupata saini ya beki huyo raia wa Ghana kwani bado ana mkataba na matajiri hao jambo ambalo inaelezwa kuwa linawapasua kichwa mabosi wa Yanga.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit aliweka wazi kuwa hakuna mchezaji ambaye wanaweza kumuachia ikiwa wanamuhitaji kwa kuwa hakuna timu yenye uwezo wa kuitikisa timu hiyo.

Kuhusu usajili ndani ya Yanga, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa hawajaanza usajili hivyo yanayosemwa ni tetesi pekee.

“Yanga hatujaanza usajili hivyo hayo yote yanayosikika ni tetesi tu hakuna ukweli katika masuala ya usajili,” amesema.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI vs MAMELOD....TAKWIMU HIZI HAPA...YANGA 'WAKIKAZA VIZURI WANATOBOA'...