Home Habari za michezo MAWAKILI WA MORRISON KUMSIMAMIA FEI TOTO DHIDI YA YANGA SC….WAZAZI WAKE WAKOMAA

MAWAKILI WA MORRISON KUMSIMAMIA FEI TOTO DHIDI YA YANGA SC….WAZAZI WAKE WAKOMAA

Habari za Yanga SC

Kimeumana! ndivyo unavyoweza kusema kuhusu sakata la mkataba wa kiungo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na uongozi wa Yanga SC, ambapo leo Ijumaa kiungo huyo ameripoti kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuitikia wito wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuhusu shauri lake la kuvunja mkataba akiambatana na mawakili waliowahi kumsimamia Morrison.

Desemba 23, mwaka jana Fei Toto aliwasilisha barua ya kuvunja mkataba na Yanga SC baada ya kurudisha kiasi cha shilingi Milioni 112 na mshahara wa miezi mitatu kuendana na matakwa ya kimkataba na kuwaaga mashabiki wa timu hiyo Jumamosi ya Desemba 24.

Hatua hii ambayo ilipingwa na Yanga SC ambao wanasisitiza bado Feisal ni mchezaji wao mpaka Mei 2024.

Morrison aliwahi kusimamiwa na mawakili katika sakata lake la kutoka Yanga SC kwenda Simba SC ambapo walishinda. Ilidaiwa Morrison alisaini Simba SC wakati bado ana mkataba na Yanga.

Chanzo chetu cha kuaminika kilicho karibu na Fei Toto kimesema kuwa, leo Ijumaa Fei Toto anataitikia wito kwa kutua katika ofisi za TFF ambapo atawakilishwa na mawakili walioshughulikia kesi ya Bernard Morrison wakati akiwa na mgogoro wa kimkataba na Yanga SC kabla ya kuibuka mshindi wa kesi hiyo.

“Ni kweli Fei Toto amewasili Tanzania kutoka Dubai kwa ajili ya kusikiliza shauri la kesi ya mkataba wake na Yanga ambayo inatarajiwa kusikilizwa leo Ijumaa kwenye Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF.

“Jambo la kushangaza ni kuwa Fei Toto atawakilishwa na mawakili ambao walikuwa wakisimamia kesi ya Morrison kuhusiana na sakata la mkataba wake na Yanga wakati anajiunga na Simba SC ambayo Morrison alishinda.

“Sambamba na mawakili hao Fei Toto pia ataongozana na wazazi wake wote wawili kwa lengo la kuhakikisha kama shauri hilo halitamalizwa , basi wazazi hao watabaki kuendelea ‘kumlinda’ mtoto wao hadi kieleweke.”

SOMA NA HII  YANGA WAIPA TFF MILIONI MOJA