Home Habari za michezo YANGA WAFANIKIWA KUIINGIZA AL MAREIKH KWENYE MFUMO

YANGA WAFANIKIWA KUIINGIZA AL MAREIKH KWENYE MFUMO

Yanga vs Namungo

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa Klabu ya Al-Merrikh ya Sudan wamekubali kuwa ni wadogo kwa Yanga SC, jambo linaloweza kuwasababishia kipigo ambacho hawatakisahau.

Yanga na Merreikh wataingia Dimbani leo pale Azam Complex kusaka tiketi ya kwenda hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika baada ya mchezo wa kwanza kunalizika kwa Yanga kushinda bao 2-0.

“Kitendo cha Kocha wa Al Merrikh kukubali kwamba mechi ya kesho (leo) anaenda kuifungua, binafsi naamini kinamuweka kwenye hatari zaidi ya kufungwa goli nyingine nyingi sana, kwa sababu Yanga ni timu ambayo fitness yake inaiwezesha kucheza kwa momentum ile ile tangu dakika ya kwana mpaka dakika ya 90.

“Kariba ya wachezaji wengi wa Sudan sio Born-Talent…sio wachezaji wale ambao wamezaliwa wakiwa na talent kubwa, lakini ni wachezaji ambao wametengenezwa kuwa wachezaji ambao wame-Fit-In zaidi kimfumo.

“Kwa hiyo ukiangalia hata namna ya uchezaji wao wana-deal sana na basic za mfumo…one touch wameondoka…touch moja pasi ipo njiani…wamekuwa wakicheza zaidi kimbinu,” amesema Wakanda Republic.

SOMA NA HII  PHIRI AFUNGUKA HAYA KUHUSU PENALTI ALIYOKOSA KWENYE NGAO YA JAMII