Home Habari za michezo POWER DYNAMO HOFU YATANDA ISHU IKO HIVI

POWER DYNAMO HOFU YATANDA ISHU IKO HIVI

Habari za Simba SC

Kikosi cha Power Dynamos kimeingia nchini jana kwa pambano la marudiano la raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Mwenya Chipepo akiingiwa na hofu juu ya wapinzani wao.

Mchezo huo wa marudiano utakaopigwa Oktoba Mosi, kwenye Uwanja wa Azam Complex utatoa taswira nzima ya timu itakayosonga mbele katika hatua ya makundi ya michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi kuanzia Novemba.

Akizungumza nasi kutoka Zambia, Chipepo alisema haitakuwa mchezo mwepesi kutokana na rekodi ya Simba, ingawa hawataingia kinyonge kwani kila mmoja wao anatambua umuhimu wa michuano hiyo mikubwa Afrika.

“Baada ya kumaliza mchezo wa mwisho sisi kama benchi la ufundi tulikaa na wachezaji na kuwajenga kimwili na kiakili kwa sababu wapo baadhi yao walishaanza kushawishika jambo ambalo kwetu halikuwa nzuri,” alisema.

Chipepo aliongeza changamoto katika mchezo huo ni nguvu kubwa ambayo mashabiki wa Simba wanayo kwani hata mechi ya kwanza Zambia waliliona hilo hivyo wanatarajia ugumu kwenye marudiano.

“Ukizungumzia Afrika Mashariki nadhani Tanzania ina mashabiki ambao wako karibu zaidi na timu zao na hilo wamelionyesha kwa vitendo kwa sababu wamekuwa nazo bega kwa bega japo tuko tayari kukabiliana na kila hali.”

Dynamos ni mabingwa wa Zambia ilifuzu hatua hiyo kwa bao la ugenini baada ya mchezo wa kwanza kupoteza mabao 2-1 dhidi ya African Stars ya Namibia kisha marudiano kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa ikashinda 1-0.

Mchezo wa kwanza dhidi ya Simba uliopigwa, Ndola Zambia na timu hizo zilifungana mabao 2-2 huku shujaa wa Simba akiwa ni Clatous Chama aliyefunga yote mawili, hivyo kuiweka timu yake kwenye mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi.

SOMA NA HII  ISHU YA NAMUNGO NA KOCHA MPYA IMEKAA HIVI