Home Habari za michezo WACONGO WAMSHTUA GAMONDI AFANYA MABADILIKO HAYA

WACONGO WAMSHTUA GAMONDI AFANYA MABADILIKO HAYA

Dakika 90 za mechi ya ugenini ya Al Merrikh ya Sudan na AS Otoho ya Congo Brazaville zimemshtua Kocha Miguel Gamondi akalazimika kuongeza nguvu ya ziada kuekelea mchezo wa leo.

Gamondi ameurudia mara kadhaa mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Stade Alphonse Massemba-Debat pale Brazzaville. Badae mechi ya Rwanda ikamalizika kwa suluhu, Merreikh wakapita.

Kwenye ile ya ugenini walitupia fasta dakika ya pili na kubadilisha staili ya uchezaji kulinda ushindi, lakini dakika ya 31 wenyeji wakajaa kambani ngoma ikaenda mapumziko 1-1 na ikaisha hivyo.

Sasa Gamondi amesema kwamba ameuangalia mchezo huo kwa umakini na akagundua ni tahadhari gani za kuchukua licha ya kwamba wana ushindi wa mabao 2 mkononi.

Al Merrikh ambayo iliwahi kuwauzia Simba, beki Pascal Wawa, itarudiana na Yanga kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam saa moja usiku huku swali kubwa la mashabiki likiwa ni staili ya uvaaji kwani siku hiyo wameombwa na viongozi iendane na ya staa wao, Aziz Ki ambaye hupenda kupandisha bukta.

Yanga imepania kulinda matokeo ya awali na kutinga makundi, kuweka rekodi kwa miaka 25. Kocha Gamondi ameshtukia pia kwamba kama wakipata matokeo kuanzia dakika ya 70 wataanza kupoteza muda.

Alichogundua kingine ni kwamba wanapokuwa ugenini huwa wanacheza zaidi soka la kushambulia tofauti na inapokuwa nyumbani na fasta amekaa na wachezaji wake kuwapa mchongo wa kuwazima Wasudani hao pale Chamazi ambako Yanga italipia Sh6 milioni kuchezea hapo mechi hiyo.

Gamondi alisema walishaukagua mkanda wa mchezo wa ugenini ambao Al Merrikh walingia kwa kasi na kuwapa presha kubwa wenyeji na kufanikiwa kupata bao la mapema licha ya wenyeji kuchomoa.

Gamond ameona ni lazima afanye kitu mapema ili kupata matokeo mazuri nyumbani na hataki mbinu za Merreikh ziwaharibie siku. Ameliambia Mwanaspoti kwamba amewapanga mabeki na viungo wacheze kazi kazi dhidi ya Merrikh ambako kwao hakuna ligi kutokana na machafuko.

Gamondi amewapa mazoezi makali mabeki wake na viungo wake jinsi ya kuongeza nidhamu ya mchezo, lakini kubwa akitaka pia timu yake itumie nafasi haraka kuwaongezea mlima wapinzani wao na aliliambia Mwanaspoti katika mchezo huo wa kesho atatumia mbinu tofauti na zile alizotumia Kigali na kushinda 2-0.

“Tunatakiwa kuwa makini nao, bado mechi haijaisha kabisa tunajua mbinu zao wanapocheza ugenini ikitokea tukaona tumemaliza tunaweza kukutana na mshtuko mkubwa tunakiwa kubaki timamu tukiishi na melengo ya kutafuta ushindi zaidi,” alisema Gamondi na kuongeza;

“Tunatakiwa tucheze kwa nidhamu kubwa ya mchezo, tumefanya mazoezi mengi ambayo yatawapa ubora vijana, haitakuwa mechi rahisi kabisa kwani hata wao wanaweza kupata matokeo ambayo tumeyapata kule endapo tu.”

Yanga inahitaji sare, ushindi wowote au isifungwe zaidi ya bao moja kubaki salama kubadilisha historia yao kwa kurejea tena Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Nahodha Bakar Mwamnyeto aliyekuwa anamuuguza Baba yake amerejea, sambamba na Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ ambaye Gamondi anajipanga kumtumia. Staa huyo hajaonekana uwanjani kipindi kirefu.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA MTIBWA SUGAR