Home news TAMBWE KUTUA LEO ..KUJIUNGA NA TIMU YA DARAJA LA KWANZA..ATUPA DONGO YANGA

TAMBWE KUTUA LEO ..KUJIUNGA NA TIMU YA DARAJA LA KWANZA..ATUPA DONGO YANGA

 


WAKATI timu ya DTB inayotarajiwa kushiriki Championship (Lidi daraja la kwanza) ikizidi kuboresha kikosi chao aliyekuwa mchezaji wa Simba na Yanga Amis Tambwe anatarajia kutua Tanzania leo Jumapili Agosti 22.

DTB moja ya timu zilizowashtua wadau wengi wa kandanda kutokana na aina ya wachezaji ambao inawasajili kwa ajili ya kuipandisha Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23.

Tambwe ambaye amekiri kurejea Tanzania kwa mara nyingine akiwa na timu ya chini akiamini kwa ushirikiano na wenzake wataipandisha.

“Nakuja Tanzania Jumapili, ni kweli nitakuwa mchezaji wa DTB, mpira ndio kazi yangu timu yoyote ikinihitaji tukakubaliana nacheza tu wala sina ubaguzi katika hilo,” alisema Tambwe.

Tambwe alisema analifahamu vizuri soka la Tanzania kwa ujumla linahitaji ushindani mkubwa na nguvu zaidi ili kuweza kufanya vizuri.

“Ligi ya Tanzania imekuwa maarufu sana na inaonekana kutokana na kutangazwa zaidi tofauti na huko nyuma, hivyo inawafanya watu wengi kuifuatilia zaidi,” alisisitiza.

Alisema yeye kama mchezaji anafarijika kurejea sehemu ambayo anajua na kutambua namna gani ya kucheza hivyo hiyo ni fahari kubwa kwake katika majukumu yake kikazi.

“Mimi namshukuru sana Mungu Tanzania najulikana sana, na watu wananitambua na wanajua kazi yangu, sina ugeni wowote na pia inawafanya watu waifuatilie hiyo timu zaidi,”

Wakati huo huo Tambwe alisema, usajili wa Yanga ni mzuri lakini cha msingi akisisitiza ligi itakapoanza ndipo watajua na kuona ubora wa waliowasajili.

“Kusajili ni kitu kingine na kufanya vizuri ni jambo lingine, ligi ikishaanza ukiwatazama wanavyocheza na matokeo wanayoyapata ndiyo yatakupa tafsiri ya usajili ulioufanya,” alisema Tambwe.

SOMA NA HII  KISA SIMBA SC KUTOLEWA CAF....YONDANI AIBUKA NA HILI JIPYA...AITAJA YANGA SC...