Home news KUELEKEA MECHI YA KESHO…NABI ANGIWA MCHECHETO DHIDI YA NAMUNGO..ADAI NI WAGUMU…

KUELEKEA MECHI YA KESHO…NABI ANGIWA MCHECHETO DHIDI YA NAMUNGO..ADAI NI WAGUMU…


Lindi. Ubora wa Namungo hasa inapocheza dhidi ya Yanga, umemfanya kocha wa wanajangwani, Nasreddine Nabi kuchukua tahadhari dhidi ya timu hiyo kesho.

Namungo itaikaribisha Yanga kesho kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika kwenye uwanja wa Ilulu Lindi.

 Nabi amesema anakutana na Namungo yenye wachezaji wazoefu na mabadiliko makubwa hivyo lazima wajipange kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

Amesema wamejiandaa vizuri kwani anajua ugumu wanaokutana nao wanapocheza na Namungo lakini anawaamini wachezaji wake kwamba watapambana na kuipa timu ushindi.

Nabi amesema Namungo ina mabadiliko mengi katika kikosi chake msimu huu hivyo lazima waikabili kwa tahadhari lakini wao kama Yanga wanataka ushindi ili kujiwekea mazingira mazuri ya kuyafikia malengo yao.

“Nawashukuru mashabiki wengi waliotupokea Jana tulipowasili Lindi na naamini watakuja kwa wingi uwanjani kuisapoti timu.

“Tumejiandaa vizuri na mchezo huo kwani yale mapumziko ya FIFA kupisha mechi za timu ya Taifa yamenisaidia kuwajenga wachezaji waliobaki kikosini kwa sababu tulipata mechi za kirafiki hivyo tuko tayari kwa mchezo kesho” amesema Nabi

“Namungo ni timu nzuri na ngumu hivyo hatakuwa mechi rahisi kwani wapinzani wetu Wana mabadiliko makubwa msimu huu.

“Nina timu nzuri yenye Wachezaji Bora hivyo naamini watapanbana kwa ajili ya kuipa timu matokeo mazuri” amesema Nabi.

Yanga haijawahi kuifunga Namungo kwenyeLigi tangu mwaka 2019 lakini imewahi kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye kombe la Mapinduzi 2021 na bao 1-0  kwenye  Kombe la Shirikisho  (FA) mwaka 2019.

Kwenye Ligi timu hizo zimekutana mara nne na mechi zote zilimalizika kwa sare.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIMNGOJA KWA HAMU MANZOKI....BUMBULI ATUPIWA VIRAGO KIMYA KIMYA...MRITHI WAKE NI HUYU HAPA....