Home Habari za michezo KISA UBUTU WA WASHAMBULIAJI KMC….HITIMANA ANG’ATA MENO KWA HASIRA NA KUSEMA HAYA…

KISA UBUTU WA WASHAMBULIAJI KMC….HITIMANA ANG’ATA MENO KWA HASIRA NA KUSEMA HAYA…


BAADA ya timu yake kushindwa kufunga bao hata moja ndani ya dakika 180 kocha mkuu wa KMC, Thiery Hitimana ametamka kuwa haridhishwi na aina ya kiwango cha washambuliaji wake kwani hawana umakini kwenye umaliziaji wa nafasi wanazotengeneza.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Hitimana alisema licha ya kikosi chake kutengeneza nafasi nyingi kwenye michezo hiyo miwili dhidi ya Yanga na Namungo walishindwa kufunga bao hata moja.

Mechi na Yanga walifungwa bao 2-0 wakati dhidi ya Namungo zilitoka suluhu ya bila kufungana na sasa wanajiandaa kucheza na Kagera Sugar ugenini Aprili Mosi.

“Hatukuwa makini kabisa kwenye michezo miwili iliyopita washambuliaji walitengeneza nafasi walishindwa kuzitumia tuna mchezo mgumu mbele nahitaji matokeo mazuri kuanzia kufunga na kuzuia,” alisema na kuongeza;

“Sijui hata wapi tatizo hili linaibuka kwani mara nyingi nimekuwa nikiwapa mbinu pamoja na kuwafundisha kwenye mazoezi jinsi ya kumalizia mipira kama ile wanayopata nje ya eneo la wapinzani lakini naona bado tatizo linaendelea,” alisema Hitimana.

Kocha huyo alisema ana wakati wa kuwasahihisha makosa wachezaji wake kabla hajakutana na wapinzani wake ambao amekiri wamekuwa na wakati mzuri mzunguko huu wa pili lakini hawampi shida kwasababu anahitaji matokeo ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kumaliza msimu vizuri.

Washambuliaji wa KMC ambao wamekuwa wakionyesha kiwango cha juu msimu huu na kufunga maboa ni Matheo Antony (4), Charles Ilanfya (3) na Hassan Kabunda (3).

SOMA NA HII  INJINIA HERSI: KUNA WATU WANAIVURUGA YANGA KUPITIA KAULI YA 'WALA MIHOGO'...