Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAANGOLA….DEWJI ATOA DILI TAMU KWA MASHABIKI SIMBA…

KUELEKEA MECHI NA WAANGOLA….DEWJI ATOA DILI TAMU KWA MASHABIKI SIMBA…

Mashabiki Simba

Mfadhili wa zamani wa klabu ya Simba, Azim Dewji amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze siku ya Jumamosi kuchangia damu ikiwa kama sehemu ya sadaka katika mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Premio De Agosto.

Zoezi hilo la kuchangia damu litafanyika Jumamosi katika hospitali ya Taifa Muhimbili saa 4:00 asubuhi.

Simba katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Angola, ilishinda 3-1.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dewji alisema mashabiki wajitokeze kwa wingi kuchangia damu kwani Tanzania bado inahitaji damu katika kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.

Dewji alisema mashabiki watakaojitokeza watapata tiketi zitakazowafanya waweze kuingia katika mchezo wa marudiano.

“Unachangia damu Jumamosi halafu Jumapili unapata tiketi ya kwenda kuangalia mchezo uwanjani,” alisema Dewji.

Upande wa mashabiki wa Simba, Abdallah Muhomba ‘Mzaramo’ alisema kutoa damu sio kwa mashabiki wa Simba tu bali hata mashabiki wa Azam na Yanga nao wana mechi hivyo wajitokeze kutoa sadaka na mambo yanaweza kubadilika.

“Mashabiki waje kwa wingi jamani, haya matokeo ya kwanza yanawezaa kubadilika tu muda wowote kikubwa tuchangie,” alisema Mzaramo.

Wakati huo huo shabiki Moses Ambrose ‘Pasi Milioni’ alisema; ”Mashabiki wajitokeze kuchangia damu na mimi nitakuwepo,

SOMA NA HII  HUKO YANGA MAMBO NI MOTO, SKUDU, NZEGELI WAPEWA MTIHANI HUU