Home Yanga SC YANGA YATAMBA KUENDELEZA MOTO DHIDI YA IHEFU

YANGA YATAMBA KUENDELEZA MOTO DHIDI YA IHEFU


UONGOZI wa kikosi cha klabu ya Yanga umetamba kuendeleza moto wa ushindi katika michezo yao yote miwili iliyosalia ya Ligi Kuu Bara, dhidi ya klabu za Ihefu na Dodoma Jiji ili kuzidi kujihakikishia nafasi ya kumaliza katika nafasi za juu za msimamo wa ligi.

Yanga inahitaji angalau pointi moja katika michezo hiyo miwili iliyosalia, ili kujihakikishia nafasi ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, ambapo watakuwa wanafikisha pointi 71, ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote iliyo chini yao.

Yanga inatarajiwa kucheza na Ihefu kesho Alhamisi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni. huku wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Desemba 23, mwaka jana.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema: β€œMaandalizi yetu hayalengi timu moja pekee, bali tunajua ratiba yetu ina michezo miwili iliyosalia kwenye Ligi Kuu Bara, ambayo ni dhidi ya Ihefu, na Dodoma Jiji. Malengo yetu ni kushinda michezo hiyo ili kumaliza katika nafasi nzuri zaidi kwenye msimamo.”

SOMA NA HII  AZAM WAJIFUA TUNISIA KWAAJILI YA YANGA