Home Habari za michezo AZAM WAJIFUA TUNISIA KWAAJILI YA YANGA

AZAM WAJIFUA TUNISIA KWAAJILI YA YANGA

Fei Toto ajiunga Azam

KOCHA Mkuu wa Azam, Youssouph Dabo ameridhishwa na kambi ya maandalizi ya msimu ya timu hiyo ‘Pre Season’ inayoendelea nchini Tunisia huku akitaka michezo mitano ya kirafiki itakayowaweka wachezaji katika hali nzuri ya utimamu wa mwili.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Tunisia, Dabo alisema anahitaji michezo hiyo akiamini itatoa nafasi ya kutengeneza muunganiko wa wachezaji.

“Kama ambavyo unajua tuna kundi la wachezaji wazawa na wale wageni tuliosajili msimu huu, kimsingi tunatumia muda huu kuwaunganisha na hilo linawezakana kwa kupata michezo mingi na yenye ushindani ya kirafiki tukiwa huku,” alisema Dabo.

Aidha Dabo aliongeza amefurahishwa na kambi hiyo kutokana na mazingira mazuri yaliyopo kwani hayana utofauti mkubwa na huku nchini.

“Hali ya hewa ni mchanganyiko kwa sababu kuna baridi na muda mwingine joto hali ambayo imewafanya wachezaji kuendana na mazingira kwa uharaka.”
Kikosi hicho kitaweka kambi ya wiki tatu na baada ya hapo

kitarejea nchini ambapo mchezo wa kwanza utakuwa ni wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga utakaopigwa Agosti 9, Uwanja wa Mkwakwani.

Azam itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza dhidi ya Yanga kwani mara ya mwisho ilipoteza bao 1-0 kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) iliyopigwa Juni 12, kwenye Uwanja huo huo wa Mkwakwani mjini Tanga.

SOMA NA HII  PAMOJA NA SIMBA KUDAIWA KUWA TAYARI WAMESHAMNASA....MPOLE AIBUKA NA HILI JIPYA....ADAI HUU NI MUDA WA MAVUNO...