Home Habari za michezo HUKO YANGA MAMBO NI MOTO, SKUDU, NZEGELI WAPEWA MTIHANI HUU

HUKO YANGA MAMBO NI MOTO, SKUDU, NZEGELI WAPEWA MTIHANI HUU

Habari za Yanga

YANGA imerudi kambini Avic Town kujiandaa na mechi za Ngao ya Jamii, zitakazopigwa kuanzia Agosti 9, huku kocha mkuu wa timu, Miguel Gamondi akiomba mechi mbili za kutesti mitambo tena kabla ya kuvaana na Azam itakayocheza nao mechi ya awali ya michuano hiyo wanaotetea taji.

Licha ya Gamondi kutoainisha timu anazotaka kucheza nao kabla ya michuano hiyo, taarifa ambazo Mwanaspoti imepenyezewa ni kwamba huenda kesho ikacheza na AS Vita iliyopo nchini kwa ajili ya pre-season, mchezo unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa Azam Complex.

Yanga tayari imecheza mechi moja ya kutambulisha mastaa wapya katika Kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na juzi ilirejea kambini kujifua kwa mechi ya Ngao na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika zote zikipigwa mwezi ujao.

Watetezi hao wa Ngao, ASFC na Ligi Kuu Bara watacheza na Azam Agosti 9 katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kisha kuifuata Asas Djibouti Telecom katika mechi ya raundi ya awali ya Liigi ya Mabingwa Afrika kati ya Agosti 18-19.

Kwa ajili ya kujiweka fiti kwa mechi hizo, kocha Gamondi alikiri kwa sasa anahitaji mechi mbili za kukiweka vyema kikosi chake kwani mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs haujamtosha kimaandalizi.

kocha huyo kutoka Argentina alisema ana wachezaji wengi wazuri lakini wanahitaji muda zaidi wa kucheza mechi ili kujenga muunganiko ambao utawafanya waweze kuwa washuindani huku akiweka wazi kuwa mechi mbili anazozitaka moja watacheza Jumamosi.

“Nahitaji mechi mbili ili kuona ubora na mapunguifu kwa wachezaji wangu mechi moja haiwezi kunipa mwanga wa kuamini kuwa nina timu nziri na ya ushindani, mbele nina mechi ngumu ambayo itaamua njia yngu ya kuanza kupata mataji,” alisema Gamondi na kuongeza;

“Usajili uliofanyika kila mmoja ameona, ila mechi moja iliyochezwa haiwezi kuwa na majibu sahihi ya kuona mwanga wa kikosi ambacho kinahitaji kutetea mataji mawili ambayo walitwaa msimu uliopita ikiwengo ngao ambayo ndio tunaanza nayo.”

Alisema mechi mbili watakazocheza zitamua namna kikosi chao kitaweza kuonyesha ushindani baada ya kutambua ubora wa mchezaji mmoja mmoja na kuwa na kikosi cha kwanza, huku AS Vita ikitajwa kuwa ni kati ya timu ambazo zitacheza na Yanga na mechi huenda ikapigwa Jumamosi hii.

SOMA NA HII  MASHUSHUSHU WA YANGA...WAPATA TAARIFA HIZI NYETI ZA RIVERS...KUMBE WANA MBINU HIZI