Home Uncategorized LIGI KUU ENGLAND IKISITISHWA JUMLA, LIVERPOOL KUPEWA UBINGWA WAO

LIGI KUU ENGLAND IKISITISHWA JUMLA, LIVERPOOL KUPEWA UBINGWA WAO


IMEELEZWA kuwa endapo kutakuwa na kipindi kirefu cha kusimamishwa Ligi Kuu ya England kutokana na kampeni ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona itathibitishwa kwamba Liverpool ndio watakuwa mabingwa kwa msimu huu wa 2019/20.

Kutokana na kusimamishwa kwa Ligi Kuu ya England mpaka Aprili 3 kumekuwa na maswali mengi kuhusu bingwa wa ligi pamoja na uwezekano wa ratiba ya kurejea kwa ligi hiyo kuwa ngumu.
Inafikiriwa kwamba kuna hatihati ya ligi hiyo kubwa kushindwa kuendelea kutokana na baadhi ya timu kutokuwa tayari kuwaruhusu wachezaji wake kucheza mpaka pale watakapoona hali imetengamaa 
Mpango wa Serikali inaelezwa kuwa ni kupeleka mbele matukio makubwa ambayo yanamjumuiko wa watu wengi ikiwa ni pamoja na masuala ya mpira jambo ambalo linaongeza hofu kwa msimu wa 2019/20 kushindwa kukamilika.
Imeripotiwa kuwa watu  798 wamethibitishwa kukutwa na virusi vya  Corona huku 11 wakifariki ndani ya England huku Mikel Arteta Kocha Mkuu wa Arsenal na kiungo wa Chelsea Callum Hudson-Odoi wakithibitishwa kuwa na virusi hivyo.
Liverpool imewaacha mbali mabingwa watetezi Manchester City kwa jumla ya pointi 25 na ushindi kwenye mechi mbili za Ligi Kuu England kwa timu hiyo iliyo chini ya Jurgen Klopp ni nafasi yao tosha kutwaa ubingwa huo.

SOMA NA HII  YANGA YAUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA