Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA APR LEO…..MASTAA YANGA WAJIFUNGA ‘MSHIPI’ MAPEMAA…..

KUELEKEA MECHI NA APR LEO…..MASTAA YANGA WAJIFUNGA ‘MSHIPI’ MAPEMAA…..

Habari za Yanga leo

Kuelekea mchezo wa leo Jumapili dhidi ya APR ya Rwanda, Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Moussa Ndaw, amesema wamekiandaa kikosi vizuri kuhakikisha kinashinda, huku akibainisha kwamba, kutakuwa na mabadiliko ya kikosi.

Kauli ya kocha huyo imekuja wakati leo Yanga itapambana na APR katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Mapinduzi utakaochezwa kuanzia saa 2:15 usiku kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

“Tumeendelea na maandalizi yetu kwa sababu kesho ni mchezo mwingine tofauti na mechi tatu zilizopita, tutaingiza timu imara zadi kesho (leo) kwa sababu michuano ni kama inaanza rasmi.

“Uliona mechi iliyopita, tulichezesha wachezaji wengi wa timu ya vijana ili kupata muda, wachezaji wengi tuliwapumzisha lakini kesho (leo) Mungu akipenda watakuwepo, timu hii kutoka Rwanda (APR) imekuwa ikicheza michuano ya Afrika mara kwa mara, lakini sisi Yanga tunaamini tutashinda.

“Kesho (leo) ni mechi ya maamuzi, kama ukishinda unakwenda nusu fainali tupo tayari kwa mchezo huo, kikubwa zaidi wachezaji wote wapo tayari na tupo tayari kuwepo hadi mwisho wa mashindano,” alisema Ndaw.

Kwa upande wa winga wa Yanga, Denis Nkane, alisema: “Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri kuhakikisha  tunafanya vizuri kuhakikisha tunatimiza kile kilichotuleta huku.

“Ukubwa wa mchezo upo tangu tunaanza mashindano ukizingatia kwamba APR ni timu kubwa katika bara letu la Afrika, ina wachezaji wenye uzoefu na wanajua umuhimu wa mchezo wa huu, kwa hiyo binafsi na kwa niaba ya wachezaji tunafahamu mchezo  hautakuwa rahisi ukizingatia hatua iliyopo ni ya watu waliofanya vizuri katika makundi.

“Kwa hiyo sisi kama wachezaji tunafahamu mchezo huo ni mgumu na tupo tayari kwenda kuipambania nembo ya klabu yetu ya Yanga.”

SOMA NA HII  CHICO USHINDI APATA MTETEZI MPYA YANGA....DAKTARI MTUNISIA AANIKA KILA KITU KINACHOMSIBU...