Home Habari za michezo AHMED ALLY:- SIMBA ILIKUWA HAINA NAMBA 6 ASILI….

AHMED ALLY:- SIMBA ILIKUWA HAINA NAMBA 6 ASILI….

Habari za Simba leo

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema usajili wa kiungo mkabaji, Babacar Sarr utaenda kutibu matatizo yote ya kiulinzi ya timu .

Ahmed amesema katika miaka ya karibuni Simba wamekuwa wakikosa namba sita asilia lakini baada ya Sarr kutua tatizo limetatuliwa.

Ahmed ameongeza kuwa tangu alivyoondika James Kotei, Gerson Fraga na Taddeo Lwanga Simba haijawahi kupata kiungo halisi wa ukabaji ndio maana wamepambana kupata saini ya Sarr.

“Sarr ni mchezaji ambaye tulikuwa tunamkosa katika timu yetu kwa muda mrefu. Tumekuwa na wachezaji wengi bora lakini hakutuwa na namba sita halisi.”

“Sasa pale kati patakuwa na Sarr, Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Khamis, imani yetu ni kwamba tutakuwa na safu bora sana ya kiungo,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  KISA VIGEZO VYA CAF...MO DEWJI APIGA CHINI DILI LA KOCHA MPYA SIMBA...AWAPA MAAGIZO HAYA BARBARA NA MAGORI..