Home Tetesi za usajili YANGA YATUA KWA RASTA WA POLISI TANZANIA

YANGA YATUA KWA RASTA WA POLISI TANZANIA


 HASSAN Nassoro, nyota aliyekuwa akicheza ndani ya Polisi Tanzania kwa sasa anawasubiri Yanga ili aweze kumalizana nao kwa ajili ya msimu ujao.

Mtu wa karibu wa rasta huyo amesema kuwa kumalizana na Polisi Tanzania kunampa fursa kiungo huyo mzawa kuweza kumalizana na mabosi hao wa Jangwani.

“Katika ofa tano ambazo anazo Nassoro zipo ambazo zinatoka kwenye timu kubwa ambapo Yanga inapewa nafasi ya kuweza kushinda vita ya kupata saini yake,” ilieleza taarifa hiyo.

Alipotafutwa Nassoro alisema kuwa ofa zipo hivyo anasubiri kuona wapi anaweza kwenda.

“Kuhusu kuwa na ofa hilo lipo hilo la Yanga siwezi kuweka wazi kwa sasa ni jambo la kusubiri ili kujua itakuaje,” amesema.

Mbali na Yanga inaelezwa kuwa Mtibwa Sugar, Kagera Sugar nao wapo kupambania saini ya nyota huyo mwenye uwezo wa kupiga mashuti ya mbali akiwa ndani ya uwanja. 

SOMA NA HII  BALAMA MAPINDUZI AREJEA KAZINI SASA