Home Habari za michezo WAKATI AKIZIDI KUTAKATA…MOSES PHIRI AVUNJA UKIMYA KUHUSU MECHI IJAYO…MASHARTI YAKE HAYA HAPA…

WAKATI AKIZIDI KUTAKATA…MOSES PHIRI AVUNJA UKIMYA KUHUSU MECHI IJAYO…MASHARTI YAKE HAYA HAPA…

Moses Phiri ajiondoa Simba SC

Mzambia kipenzi cha Wanasimba, Moses Phiri ametoa angalizo zito kwa wachezaji wenzie na mashabiki wa Simba kuelekea mechi dhidi ya De Agosto Jumapili ijayo.

Staa huyo amewaambia kwamba wasibweteke na matokeo ya ushindi wa ugenini wa mabao 3-1 kwani katika michuano hiyo uzoefu unaonyesha lolote linaweza kutokea muda wowote iwe nyumbani au ugenini na kubaki na majuto makubwa.

Amewasisitiza kwamba kila mmoja kwa nafasi yake apambane kuongeza ushindi kwenye mchezo wa marudiano na kujidhatiti mpaka kipyenga cha mwisho kipulizwe na wajihakikishie kwamba wamekamilisha kazi moja ya kufuzu makundi ndipo waanze mipango mingine.

Nyota huyo aliyefunga bao moja katika ushindi huo wa ugenini, alisema bado wana kazi kubwa ya kufanya ili kuendeleza kiwango bora wakati watakaporudiana na wapinzani wao Jumapili Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Phiriambaye mitandao ya thamani za wachezaji inasema anauzwa Sh226Milioni, alisema ushindi huo umewapa morali kubwa; “Ni ngumu sana kushinda ugenini hasa kwenye michuano mikubwa kama hii ya Afrika, kikubwa ambacho kimetubeba ni kila mmoja wetu kujitoa zaidi kwa ajili ya timu jambo lililotupa tulichokikusudia,” alisema Phiri aliyewahi kucheza Ureno na Zambia.

“Tuna dakika nyingine 90 za kukamilisha azma yetu tuliyoianzisha tangu mwanzo, tunahitaji kujipanga vizuri na kutumia kila nafasi tutakayoipata kwani mchezo bado ni mgumu hivyo tutacheza kama hatujashinda ugenini.” alisema Phiri mwenye urefu wa futi 5.7.

Phiri ndiye kinara wa mabao katika kikosi hicho hadi sasa kwenye mashindano yote kwani michezo minane aliyocheza amefunga mabao nane akiwa na wastani wa kufunga bao moja kwenye kila mchezo na kumfanya kuendelea kung’ara. Michuano ya Caf amefunga mabao manne na Ligi Kuu manne.

Staa huyo ambaye ni usajili wa kwanza kwenye timu hiyo msimu huu akitokea Zanaco ya kwao akikitumikia alifunga mabao 14 msimu wa mwisho. Aliyekuwa Mwenyekiti wa timu hiyo, Ismail Aden Rage aliwapongeza wachezaji; “Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao, wasione kama kazi imeisha bali wajue lolote linaweza kutokea kwenye mpira wa miguu, kujitokeza kwao na kushangilia kutazidi kuwapa ari kubwa wachezaji.”

Aidha Rage alimpongeza Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Juma Mgunda kwa kazi kubwa anayoifanya huku akiweka wazi sababu kubwa ya timu hiyo kufanya vizuri chini yake ni kujiamini na kumpa kila mchezaji nafasi ya kucheza.

Lengo kubwa la Simba msimu huu ni kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kusota kwenye robo kwa misimu kadhaa mfululizo.

SOMA NA HII  GAMONDI AMTAKA STRAIKA MWINGINE, MAMBO BADO SANA