Home news KOCHA SIMBA AMTAJA KIUNGO WA DODOMA JIJI ALIYEMVUTIA

KOCHA SIMBA AMTAJA KIUNGO WA DODOMA JIJI ALIYEMVUTIA


KWA mara ya kwanza, Kocha Mkuu wa Simba, raia wa Ufaransa, Didier Gomes Da Rosa, ametoa kauli ya kuonyesha wazi kuvutiwa na uchezaji wa kiungo mshambuliaji wa Dodomajiji, Dickson Ambundo.

Juzi Jumatano, Gomes alikiongoza kikosi chake kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), ambapo Simba ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, baada ya kuibuka na ushindi mbele ya Dodoma Jiji mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Championi Ijumaa baada ya mchezo huo kumalizika, Gomes alikishukuru kikosi chake kwa kufanikisha malengo yake ya kuingia hatua ya nusu fainali, lakini aliwapongeza Dodoma Jiji kwa mchezo mzuri huku akikiri wazi kuvutiwa na uchezaji wa Ambundo.

β€œMchezo wetu haukuwa rahisi kama wengi wanavyodhania baada ya kupata ushindi, kimsingi niwapongeze wachezaji wangu kwa kufikia lengo la kuingia hatua hii, ila pia niwapongeze wapinzani wetu Dodoma Jiji kwa mchezo mzuri, ila nimevutiwa zaidi na kiungo wao mshambuliaji Ambundo.

β€œUchezaji wa kiungo huyo, unaonyesha kujua zaidi majukumu yake uwanjani na ndiyo maana utaona alitusumbua kiasi cha kunifanya nifikirie kwa umakini namna ya kumdhibiti na ndiyo maana niliingiza viungo kama Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin na Thadeo Lwanga,” alisema Gomes.

SOMA NA HII  MAGUFULI KUAGWA DAR KESHO, KUZIKWA CHATO MACHI 25 - VIDEO