Home Ligi Kuu KOCHA KAGERA SUGAR APIGIA HESABU MECHI ZAKE NNE

KOCHA KAGERA SUGAR APIGIA HESABU MECHI ZAKE NNE


 KOCHA Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Francis
 Baraza, amefunguka kuwa ameweka mkakati wa kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mechi nne zilizosalia ili wajinusuru na janga la kushuka daraja msimu huu.

Kagera Sugar inapambana kujinasua na janga la kushuka daraja kutokana na kuwa na mwenendo usioridhisha kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kukusanya pointi 33 kwenye mechi 30 walizoshuka dimbani hadi sasa, wakiwa katika nafasi ya 13.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Baraza alisema: “Tunaendelea na maandalizi kuelekea mechi zetu za mwisho ambazo zimebakia, najua ugumu ambao upo kwenye ligi kutokana na kila timu kupambana kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutoshuka daraja.

 “Kwenye mechi nne ambazo tumebakiwa nazo ni lazima tupambane kuhakikisha tunapata matokeo ili tuweze kujinusuru na janga la kushuka daraja.”

Kagera Sugar imebakiza mechi nne kumaliza Ligi Kuu Bara msimu huu ambazo watashuka dimbani dhidi ya Polisi Tanzania, Prisons, Ihefu na Coastal Union.

SOMA NA HII  MATOKEO YA MECHI ZA LEO NDANI YA LIGI KUU BARA