Home Uncategorized NGASSA: TUTAPAMBANA KIUKWELI MSIMU UJAO

NGASSA: TUTAPAMBANA KIUKWELI MSIMU UJAO


KIUNGO mshambuliaji  wa Yanga, Mrisho Ngassa amesema kuwa anafuraha kuona anaendeleza makali yake ndani ya kikosi hicho na anaamini watapambana kiukweli msimu ujao.

Ngassa jana alifunga hat trick kwenye ushindi wa mabao 10-1 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzanite FC uliochezwa uwanja wa Highlands Parks, Moro.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ngassa amesema kuwa ni mwanzo mzuri kwake na timu pia kwa ajili ya msimu ujao.

“Ni mwanzo mzuri kwetu na timu kiujumla, imani yetu ni kuendela kupambana kwa ajili ya msimu ujao,” amesema Ngassa.

SOMA NA HII  WANA KINONDONI BOYS 'KMC' HAWALALI, WASAJILI MASHINE SABA MIAKA MITATU