Home news BAADA YA KUIZOEA TIMU MPYA…NKANE AFICHUA SIRI ZA YANGA HADHARANI…AANIKA HOFU ALIYONAYO…

BAADA YA KUIZOEA TIMU MPYA…NKANE AFICHUA SIRI ZA YANGA HADHARANI…AANIKA HOFU ALIYONAYO…


KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga, Denis Nkane amefichua kuwa miongoni mwa mambo ambayo kila staa wa timu hiyo anafikiria kwa sasa ni kuhakikisha anacheza kwa kiwango kikubwa, ili kufanikisha malengo yao ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mpaka sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara Yanga ndiyo vinara na pointi zao 35 walizokusanya katika michezo 13, ambapo kiwango kikubwa wanachokionyesha kimefanya wapewe nafasi kubwa ya kumaliza ukame wa misimu minne bila ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Nkane ambaye alijiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili akitokea Biashara United ya Mara, alikuwa nje ya uwanja kwa muda kufuatia kuwa na majeraha lakini sasa amesharejea.

Akizungumza na gazeti la Championi Ijumaa, Nkane alisema: “Nashukuru Mungu kwa kupona na kuanza mazoezi pamoja na wenzangu tayari kwa ajili ya kuendelea kuipambania timu katika malengo yetu makubwa ya kushinda ubingwa katika michuano ambayo tunashiriki.

“Nilipokuwa nje nilikuwa na hofu kutokana na ukweli kuwa kwa kikosi chetu cha sasa kadiri unavyozidi kukaa nje ndivyo unajiweka kwenye nafasi ngumu ya kurudi kikosini, kwani kila mchezaji anachowaza ni kupambania nafasi na kuhakikisha tunashinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUSAJILIWA KWA MBWEMBWE...STRAIKA MPYA YANGA AIBUKA NA KUWEKA HADHARANI MAMBO HAYA...