Home Uncategorized NYONI ATIMIZA AHADI YAKE KWA SHABIKI WAKE NAMBA MOJA

NYONI ATIMIZA AHADI YAKE KWA SHABIKI WAKE NAMBA MOJA

ERASTO Nyoni nyota wa Simba leo Agosti Mosi ametimiza ahadi kwa shabiki yake Jumanne Ulimwengu ya kumnunulia baiskeli ambayo ataitumia kwenda shule.

Nyoni alitoa ahadi hiyo jana, Julai 31 wakati akimkabidhi zawadi ya jezi mtoto huyo.

Ulimwengu alikuwa amevaa jezi ya Nyoni ikiwa imechorwa jina lake na namba ya Nyoni jambo lililomfanya beki huyo ampe zawadi ya jezi pia aliomba apewe baiskel ili aitumie kwenda shule jambo ambalo Nyoni aliahidi kulitimiza na leo limetimia.

Simba ipo Sumbawanga ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC itakayochezwa kesho, Agosti 2, Uwanja wa Nleson Mandela.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA HANA CHAGUO LA KWANZA