Home KMC FC KMC WAREJEA KAMBINI, KAZI IMEANZA SASA

KMC WAREJEA KAMBINI, KAZI IMEANZA SASA


WACHEZAJI wa KMC leo wameanza mazoezi rasmi kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

KMC ilitoa mapumziko kwa wachezaji wake kuanzia Mei 17 mpaka Mei 25 baada ya timu hiyo kutokuwa na mchezo wowote wa mashindano ambapo inapambana kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

 Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya KMC,Christina Mwagala, amesema: “Tulitoa mapumziko kwa wachezaji tangu Mei 17 hadi Mei 25, tayari kikosi kimeingia kambini kujiandaa na mechi zetu zilizobaki.

“Hii itakuwa maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji ambao unatarajiwa kuchezwa Mei 17, katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambao ninaamini utakuwa mchezo mgumu lakini tutapambana kuweza kupata matokeo ili tuweze kufufua matumaini ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo, ” .

Timu hizo zilipokutana katika mzunguko wa kwanza Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Desemba 4, KMC ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 huku Dodoma Jiji wakifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa raundi ya tano ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Mei Mosi jijini Dodoma.

Dodoma Jiji imeishia hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba kwenye robo fainali, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  JESHI KAMILI LA KMC 2021/22 HILI HAPA