Home Habari za michezo JE NABI ATAFUA DAFU MBELE YA MBRAZIL SIMBA…UKWELI HASWAA HUU HAPA

JE NABI ATAFUA DAFU MBELE YA MBRAZIL SIMBA…UKWELI HASWAA HUU HAPA

Habari za Yanga SC

Mechi inayobeba chapa ya ligi ya Tanzania bara, zinakutana timu mbili ambazo zimekuwa na kiwango kizuri kinachoambatana na matokeo mazuri katika mechi zao za hivi karibuni.

ROBERTINHO.
Inatosha kusema ameshaanza kupata kile ambacho alikuwa anakihitaji kwa wachezaji wake tactically, katika mechi za mwanzoni Simba haikuwa na performance nzuri chini yake, alihitaji kuona Simba ina press hasa kwa mistari yake miwili ya mbele inayotengeza umbo la (1-4/1-3 au 2-3), haya wayafanye wakatil wapinzani wanafanya build up.

Simba ilikuwa inapata shida kwa sababu hawakuwa na ufanisi wanapofanya press kuanzia juu, wanapofikiwa kwenye kiungo ilikuwa ni rahisi kuwafungua kwa sababu walikuwa wanabaki wachache na kujikuta wapinzani wananufaika kwa kuwa wengi (numerical advantage ), kitu kizuri kwa sasa Simba wamekuwa wagumu kuwafungua kwa sababu mistari yao miwili ya juu inatekeleza vizuri mpango mkakati namba moja wanapozuia.

Simba ni untouchable wanaposhambulia, wanatengeneza overloads katika zone ya mpinzani 4-2-4 au 4-2-2-2 kama wataamua kuliziba eneo lao la katikati ili kuzuia vizuri counter attacks, ingawa kuna nyakati wanashambulia wakiwa na wide playmakers au namba kumi wawili (CAM’s).

NABI.
Mwalimu mgumu kukabiliana nae, ni moja ya walimu bora tactically na anapewa back up na quality ya wachezaji wake, msingi wake wa kwanza ni kucheza kuanzia chini, utamu wa mechi unaweza kuwa hapa, nani ambae ataweza kumzuia mwenzake katika wakati ambao anafanya build up.

Yanga wanakuwa na wachezaji watatu nyuma wanapofanya build up, Djigui, Job na Bangala/Bakari, kidogo kwa Bakari anazikosa pasi hatari lakini kama wanacheza Job na Bangala maana yake pasi yao moja inaweza kuvunja mistari hata miwili ya wapinzani.

Yanga wanashambulia sana kupitia pembeni na kati, wanatengeneza nafasi kupitia huko, wanaweza kuweka mtego wao kwa kukimbia nyuma ya walinzi wa pembeni wa Simba, utofauti wa mchezo huu mara nyingi timu zinaogopa kufungulia busta, kila mchezaji anafikiria kwanza kuisaidia timu yake isiruhusu bao na hii inawapunguzia ufanisi wanapotakiwa kushambulia.
It’s a DABIIII

SOMA NA HII  HII HAPA MASHINE YA SIMBA YARUDI UWANJANI...NI BAADA YA KUKAA NJE MUDA MREFU