Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA KUKIWASHA ….MAXI NZENGELI ATAJA JAMBO ANALOLITAKA KWA YANGA…

BAADA YA KUANZA KUKIWASHA ….MAXI NZENGELI ATAJA JAMBO ANALOLITAKA KWA YANGA…

Habari za Yanga

KIUNGO wa Yanga, Maxi Nzengeli ameweka wazi kulingana na program wanayopewa na Kocha Miguel Angel Gamondi ni suala la muda kukata kiu ya mashabiki wao kuona timu yao ikicheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ili wafanikiwe kutinga katika hatua ya makundi ya michuano hiyo wanatakiwa kuhakikisha wanaiondoa Al Merrikh, mchezo unaofuata wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Septemba 16, mwaka huu.

Max alisema malengo yao ni kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kufikia malengo yao ya kufika hatua ya makundi.

Alisema malengo yake anaisaidia Yanga kufika kwenye malengo kwenye michuano hiyo kwa kufika katika hatua ya makundi huku akiamini kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwaondoa Al Merrikh.

“Malengo ya timu ndio ya wachezaji wote, kwetu tunatamani kuona tunafika makundi na kupita zaidi ya hapo, kikubwa tunachokifanya kwa sasa ni kuona tunapambana zaidi kwenye michezo yetu.

“Kocha anaendelea kufanya majukumu yake ya kuendelea kufanyia kazi makosa aliyoyaona kwenye mechi zilizopita, tunashinda michezo yetu miwili iliyo mbele yetu dhidi ya Al Merrikh,” alisema Nzengeli.

Alisema muhimu zaidi kwa upande wetu kuona wanafanya vizuri na kupata matokeo, kuna uwezo huo na tutapambana zaidi kufikia malengo yao .

Nzengeli alisema anaimani ya timu yake kufanya vizuri katika mashindano ya ligi ya Mabingwa Afrika na kuona Yanga ikitinga makundi kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa.

SOMA NA HII  KUHUSU MICHUANO YA CAF...ALEX SONG AIPIGIA 'UPATU' SIMBA...AFUNGUKA MATAMANIO YAKE YA MOYONI.....