Home Habari za michezo BAADA YA KUONA KAMA ANASAHULIKA HIVI….SKUDU KAIBUKA NA HILI JIPYA YANGA…

BAADA YA KUONA KAMA ANASAHULIKA HIVI….SKUDU KAIBUKA NA HILI JIPYA YANGA…

Habari za Yanga SC

Winga wa Yanga kutoka Afrika Kusini, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’, amesema amegundua mbinu mpya ya kupata muda zaidi wa kucheza kikosini.

Skudu aliyeanza kukitumikia kikosi hicho msimu huu akitokea Marumo Gallants, katika mahojiano yake  hakuacha kuvimba kuhusu timu yao ya Taifa inavyofanya vizuri kwenye Afcon.

Kuhusu Yanga,alisema kuwa kuhusu nafasi yake bado anaendelea kuipambania nafasi yake ndani ya kikosi hicho licha ya ushindani mkubwa wa namba uliopo lakini anaamini kwasasa njia zimefunguka na ameshajua cha kufanya kuongeza wigo wake.

Alikiri kuwa kutokana na ubora wa wachezaji waliopo katika timu sasa amerudi raundi ya pili ya msimu na mbinu mpya kabisa ili kuhakikisha anatoboa na haoni kitakachomzuia.

“Kwa ushindani uliopo nimegundua kuwa ili niweze kuwa na nafasi zaidi lazima nifanye kitu cha tofauti kila ninapopata nafasi.Kila kocha atakaponipa nafasi lazima nionyeshe kuwa nilistahili kwa kufanya jambo ili kuweza kumfanya mwalimu anipe namba zaidi,” aliongeza kuwa tayari pia ameshaizoea ligi tofauti na awali.

Alieleza kuwa kama utani timu yao ya Bafabafana imepasua na watu wasishangae wakichukua taji la Afrika kwani wana kipa na kikosi bora sana.

“Kipa tuliyenaye namjua na timu ya Taifa na kikosi cha Mamelodi kimekuwa kwenye mapambano ya kumsuka kufikia kiwango hicho alichonacho, ni mlinda mlango mzuri sawa na Djigui Diarra,”alisema.

SOMA NA HII  SIMBA YA ROBERTINHO NI HATARI KILA NAFASI NI BAO