Home Yanga SC BREAKING:DAVID BRYSON ATAMBULISHWA YANGA

BREAKING:DAVID BRYSON ATAMBULISHWA YANGA

 


RASMI sasa leo Agosti 12, Yanga wamemtambulisha nyota wao mpya David Bryson ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya KMC.

Beki huyo wa kushoto ni moja ya waliokuwa tegemeo ndani ya KMC anaungana na mzawa mwingine Dickson Ambundo ambaye alitambulishwa jana Agosti 11.


Ni dili la miaka miwili amesaini kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi ambao wapo chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.

Kikosi hicho kinatarajia kwenda kuweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa bado usajili unaendelea na kwa sasa ni nyota wawili wa kimataifa wamebaki kutambulishwa rasmi.

SOMA NA HII  KUMBE MKUDE SIO JEZI NAMBA 6 WA YANGA, ALLY KAMWE AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU NAMBA SITA NA UJIONWAKE ISHU IKO HIVI