Home Habari za michezo KAPOMBE:- LEO KAZI NI MBILI TU…

KAPOMBE:- LEO KAZI NI MBILI TU…

Habari za Simba leo

Beki wa kulia wa timu ya Simba, Shomari Kapombe amesema kuwa wamejiandaaa vizuri kwa ajili ya mchezo wao wa dabi dhidi ya watani zao yanga SC utakaopigwa leo Aprili 20 katika Dimba la Mkapa.

Kapombe amesema kuwa malengo yao ni kushinda mchezo huo, hivyo kocha amewaelekeza mambo yote muhimu ya kufanya ili kutoka na ushindi huku akisahihisha makosa ya wachezaji wake ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara.

“Tumejiandaa vizuri na wachezaji wote tuna ari nzuri ya kucheza mchezo wa kesho(leo). Tunachoshukuru ni kwamba mwalimu amepata muda mrefu wa kuiandaa timu katika nyanja zote ili kufanya vizuri katika mchezo wa leo.

“Sisi kama wachezaji tuko tayari kwenda kupambana kwenye mchezo huo, kuhakikisha tunacheza vizuri na kupata matokeo mazuri. Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha tunafuata maelekezo ya mwalimu ndani ya uwanja. Tunafahamu ni kiasi gani mashabiki zetu wanazitaka alama tatu .

“Kwa hiyo la kwanza ni kufuata maelekezo aliyotupa mwalimu na pili ni kuchukua majukumu ambayo wanaSimba wanataka alama tatu, tukiunganisha tunapata nguvu ya kuzipambania alama tatu ” amesema Kapombe.

SOMA NA HII  KISA SAWADOGO...MAFISANGO AKUMBUKWA SIMBA...ISHU NZIMA IKO HIVI...