Home Habari za michezo HUYU MZAMIRU MPYA NI BALAA NA NUSU…KWA TAKWIMU ZAKE HIZI NDIO MAANA...

HUYU MZAMIRU MPYA NI BALAA NA NUSU…KWA TAKWIMU ZAKE HIZI NDIO MAANA MGUNDA KAMGANDA…

KIUNGO wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba, Mzamiru Yassin ni habari nyingine eneo la kati kutokana na kuimarika kwenye kila mchezo ambao ataanza.

Nyota huyo kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars alikuwa na majukumu matatu, kupoka mipira kwa wapinzani, kulinda na kupeleka mashambulizi kwenye lango la wapinzani.

Asilimia 80 ya mipira aliyokuwa anapiga ilikuwa inafika kwa walengwa husika na kutokana na kazi ngumu aliyofanya alichezewa faulo dakika ya 19 na 37 na aliyeyusha dakika zote 90 bila kuonyeshwa kadi ya njano.

Kwenye ligi kacheza mechi 8 kayeyusha dakika 526, kafunga bao moja na katoa pasi moja ya bao msimu wa 2022/23 ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUIFUNGA TZ 3-0....KOCHA WA MOROCCO AFUNGUKA ALICHOKIONA KWA STARS....