Home Habari za michezo HAYA HAPA MAGOLI YA AJABU YALIYOFUNGWA LIGI KUU TANZANIA

HAYA HAPA MAGOLI YA AJABU YALIYOFUNGWA LIGI KUU TANZANIA

TIKETI MECHI YA YOUNG AFRICAN(YANGA) VS US MONASTIR...FULL HOUSE FULL SHANGWE...MWANANCHI UPO TAYARI?

Mambo yanazidi kuwa magumu kwa The Tigers Queens ya Arusha baada ya kupokea kipigo kingine kikubwa jana kwenye Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

Tigers imefungwa mabao 4-1 na Alliance Girls katika mchezo wa raundi ya 12 ya ligi hiyo ambao umepigwa jana kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza baada ya kuahirishwa juzi.

Mabao ya Alliance yamefungwa na Winfrida Charles aliyepachika kambani mawili dakika ya 20 na 71, Moga Patrick dakika ya 15 na Shufaisa Issa dakika ya 90 huku bao la kufutia machozi la Tigers likifungwa na Zeyonce James dakika ya 25 kwa mpira wa kutengwa uliozama wavuni.

Kichapo hicho kikubwa ni cha pili mfululizo ndani ya wiki mbili ambapo mchezo uliopita ilichapwa mabao 7-0 na Simba Queens.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Alliance katika michezo minne iliyopita kwenye ligi baada ya sare ya 0-0 na Baobab Queens na Amani Queens kisha ikachapwa 4-3 na Ceassia Queens.

Ushindi wa mabao 4-1 ambao imeupata leo Alliance Girls ni sawa na ilioupata kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Tigers uliopigwa katika Uwanja wa Black Rhino, Karatu.

Mabao mawili ambayo amefunga leo Winfrida Charles anafikisha
jumla ya mabao nane katika michezo 12 ya Ligi Kuu, akiwa kinara wa mabao kwa timu hiyo huku akikamata nafasi ya tatu.

kwenye ligi nyuma ya Jentrix Shikangwa wa Simba (10), Cynthia Musungu na Oppah Clement (9) ambao tayari wametimkia barani Ulaya.

Kufuatia ushindi huo, Alliance imepanda hadi nafasi ya tano ikifikisha pointi 17 huku Tigers ikibaki kwenye nafasi ya nane na pointi zao saba baada ya michezo 12.

SOMA NA HII  YANGA WAPINDUA MEZA KIBABE KWA FEI TOTO...WAMALIZANA NAYE MAZIMA..SASA KUPEWA MSHAHARA ML 15..