Home Habari za michezo WAZIRI “MWANA FA:- AWAFUNGA MDOMO TFF…NDONDO CUP 2023 ITAFANYIKA

WAZIRI “MWANA FA:- AWAFUNGA MDOMO TFF…NDONDO CUP 2023 ITAFANYIKA

WAZIRI

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema kuwa Mashindano ya Ndondo Cup yanayoratibiwa na mtangazaji Shaffih Dauda yatafanyika.

Kauli ya kiongozi huyo wa Serikali imekuja ikiwa ni siku moja baada Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusema kuwa shindano hilo halijapata kibali cha mamlaka hiyo ili liweze kufanyika.

Mwana FA amesema jambo hilo halina ugumu wowote kwani taratibu zitafuatwa na litafanyika kwa kuwa muda bado upo wa kutosha na kuondoa sintofahamu kwa walioamini huenda Ndondo Cup isifanyike mwaka huu.

SOMA NA HII  YANGA INAGAWA DOZI NYUMBANI NA UGENINI...GARI LIMEWAKA JANGWANI...MNYAMA HAFUI DAFU