Home Uncategorized LIVERPOOL IMEBEBA MATUMAINI KIBAO KUTAWALA SOKA LA ENGLAND

LIVERPOOL IMEBEBA MATUMAINI KIBAO KUTAWALA SOKA LA ENGLAND


BEKI kisiki wa Liverpool, Virgil van Dijk, amewaonya wapinzani kuwa timu yao ndio kwanza inaanza kutawala soka la England na wanatarajia watatamba kwa miaka kadhaa ijayo.
Liverpool chini ya Jurgen Klopp ilimaliza nafasi ya pili kwenye Premier msimu uliopita na kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Dunia la Klabu, na sasa inaelekea kutwaa ubingwa wa Premier kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 30.
“Tunatumaini tupo katika hali nzuri ya kumalizia kazi tuliyoianza. Kitu cha muhimu zaidi maishani ni afya na sote tulilazimika kukabiliana na kusimamishwa kwa ligi,” alisema Van Dijk.
Van Dijk alituma ujumbe kwa mashabiki kuwa, licha ya kuwa kileleni kwa tofauti ya zaidi ya pointi 22, ndio kwanza wanaanza safari ya kulitawala soka la England.

“Najua ni kwa muda gani mashabiki wamesubiria mafanikio haya.Lakini bahati mbaya hawawezi kuwepo kama itatokea tumetwaa ubingwa.
“Tukishinda mechi mbili tu sisi ni mabingwa, lakini hatutaishia hapo. Tunataka kuendelea mbele, tunataka kulibakiza kombe hata msimu ujao ambao utaanza haraka baada ya mechi ya mwisho ya msimu huu.
Kocha ameshatuambia kwamba, tutakachokifanya kwenye mechi tisa zilizobaki, kitatupa muongozo kuelekea msimu ujao.
Tunataka kuendelea kujiboresha. Tuna wachezaji ambao wanaweza kuwa bora zaidi. Kama tukitwaa ubingwa, tutataka kuutetea msimu ujao
SOMA NA HII  TFF KUZIPIGA PANGA TIMU ZA TPL MSIMU