Home Uncategorized JEMBE LINALOTUA SIMBA NI NOMA, YANGA WALISHINDWANA NAYE KWENYE MKWANJA

JEMBE LINALOTUA SIMBA NI NOMA, YANGA WALISHINDWANA NAYE KWENYE MKWANJA


NYOTA wa zamani wa Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda Michael Sarpong, amekubali kujiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya uongozi wa timu hiyo kukamilisha mazungumzo na wakala wake, huku dau lake likitajwa kuwa ni Sh milioni 138.
Sarpong raia wa Ghana, kwa sasa ni mchezaji huru baada ya Rayon kuvunja mkataba naye kwa madai ya mshambuliaji huyo kukorofishana na rais wa timu hiyo kufuatia kupunguziwa mishahara wachezaji kutokana na janga la Corona.

Mshambuliaji huyo mwenye uwezo pia wa kucheza winga zote mbili, amekuwa akiwaniwa vikali na vigogo wa soka Tanzania, Simba na Yanga.
Baada ya vita ya wawili hao kuwa kubwa hapo awali, Yanga wakajiweka pembeni baada ya kutajiwa dau kubwa huku Simba ikiendelea na mazungumzo kabla ya kukamilisha dili hilo. Taarifa za uhakika kutoka Rwanda zinasema kuwa, mshambuliaji huyo ni mali ya Simba hivi sasa baada ya kukamilisha mazungumzo ya mkataba wa miaka miwili huku dau lake likiwa dola 60,000 (Zaidi ya Sh milioni 138
“Ukweli ni kwamba Simba washamalizana na Sarpong, atajiunga nao kwa mkataba wa miaka miwili na kila kitu kimeshakamilka, dau lake ni dola 60,000 kama walivyokubaliana,” kilisema chanzo hicho kutoka Rwanda.

 Meneja wa mchezaji huyo, Alex Kamanzi amesema: “Ni kweli tumefikia sehemu nzuri na Simba na wakati wowote tutaweka wazi, lakini watu wafahamu tu kwamba kila kitu kipo sawa.
“Yanga tuliachana nao kwa sababu walikuwa na pesa ndogo tofauti na ile ambayo tulikuwa tunaitaka sisi, ndiyo maana tukawapa nafasi Simba walioonesha nia kweli ya kuihitaji huduma ya mchezaji wangu, hivyo wakati wowote tutakamilisha hili suala na kutangazwa rasmi.
Hivi karibuni, Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, alisema, katika suala la usajili, watahakikisha wanasajili wachezaji kulingana na matakwa ya kocha wao na hawatashindwa kwa vyovyote.Ujio wa mshambuliaji huyo utaifanya safu ya ushambuliaji ya Simba kuongezewa nguvu zaidi baada ya hivi sasa kuwategemea Meddie Kagere na John Bocco.
SOMA NA HII  VIGONGO VINNE VYA MOTO KWA YANGA HIVI HAPA