Home Habari za michezo RASMI…..SIMBA WAKUBALI YAISHE KWA INONGA….WATAJA BEI WANAYOTAKA KUMUUZA…

RASMI…..SIMBA WAKUBALI YAISHE KWA INONGA….WATAJA BEI WANAYOTAKA KUMUUZA…

Habari za Simba

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa endapo itakuja ofa kubwa ya mabilioni ya fedha watatengeza msimamo na kuzungumza na klabu ambayo inahitaji huduma ya beki wao wa kimataifa, Enock Inonga Baka.

Hivi karibuni kuna taarifa kuwa  kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi anayekinoa kikosi cha AS FAR Rabat ya Morocco anahitaji huduma ya beki  kisiki wa Simba,  kwa lengo la kukuiongezea nguvu kikosi chake kinachoshiriki Ligi Kuu ya nchini hiyo maarufu kama Botola Legue.

Pia inadaiwa Al Ahly ya Misri nao wameonyesha nia  kumtaka beki huyo mwenye thamani ya Dola laki tano ambayo sawa na shilingi bilioni 1.2 ambaye amebakisha mkataba wa mwaka mmoja ndani ya timu hiyo.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba,  Ahmed Ally amesema hawajapokea taarifa kutoka klabu yoyote ambayo inahitaji mchezaji wao huo na kwa sasa hawako tayari kumuuza.

Amesema licha ya kuweka tahadhari juu ya mchezaji huyo aliyekuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa lake DR Congo kutouzwa lakini watabadilisha msimamo wao huo endapo kutatokea timu imeenda na ofa kubwa.

“Inonga yupo kwenye majukumu nchini Ivory Coast  na timu ya Taifa katika michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika wametinga hatua ya robo fainali,  hakuna ofa iliyofika kwenye meza yetu licha ya sisi kuona hizi taarifa za kutajwa FAR Rabat na Al Ahly katika mitandao.

Ninachosema watu waogope matapeli. Kama kuna ofa kubwa tunazungumzia mabillion yakija mezani kwetu hilo ni suala lingine na litazungumzika,” amesema Ahmed.

Kuhusu kiungo wao Clatous Chama kusamehewa na kujiunga kambini, Ahmed amesema taarifa juu ya nyota huyo wataiweka wazi kwa sababu alisimamishwa kwa maslahi ya klabu pamoja na mchezaji husika.

“Kuhusu taarifa za Chama tutaweka wazi  ni mchezaji wetu, kama amesamehewa au bado anaendelea na adhabu yake ya utovu wa nidhamu hilo tutaliweka wazi,” amesema Ahmed.

Licha ya Simba kutoweka wazi juu ya kiungo huyo lakini inaelezwa kiungo huyo amesamehewa na kupewa onyo kali na amerejea kikosini kujiunga na wenzake kujiandaa na michezo iliyopo mbele yao ikiwemo ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mashujaa FC,  Tabora United na Azam FC mechi za viporo.

SOMA NA HII  MATAJIRI YANGA WAAMUA KUFANYA KWELI ISHU YA MORRISON...WAMPA MKATABA WA KIMKAKATI...SIMBA WAKODOA MACHO..