Home Habari za michezo SAA CHACHE BAADA YA KUTAMBULISHWA YANGA…GUEDE KAIBUKA NA HILI JIPYA…

SAA CHACHE BAADA YA KUTAMBULISHWA YANGA…GUEDE KAIBUKA NA HILI JIPYA…

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Joseph Guede ameweka wazi zoezi lake la kwanza ndani ya klabu yake hiyo ni kufanya makubwa kwa sababu Yanga ni timu kubwa yenye malengo ya kufanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yao ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Guede ametambulishwa rasmi jana katika mechi ya kombe la FA, Yanga ilipocheza mchezo wa hatua ya 32 bora dhidi ya Hausing FC, uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Dar-es-Salaam, kwa kushinda mabao 5-1.

Guede amesema amefurahi kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga, viongozi ni wazuri na wana ushirikiano ambao upo ndani ya klabu hiyo hivyo  anamini kila kitu kitakuwa sawa.

Amesema ana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha anakata kiu ya mashabiki kwa kuipatia mabao timu hiyo, kwa sababu anafahamu hilo ndio jambo kubwa ambalo Wananchi wanalisubiri kutoka kwake.

“Mbali na yote naweza kusema nimepokelewa vizuri nina furaha sana kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga, niko tayari kwa upande wangu, unajua unapokuwa ndani ya klabu sio tena kwangu binafsi nipo hapa kwa ajili ya Yanga.

Nitafanya kila liwezekanalo ili timu iweze kushinda mataji , ninaimani kwa wachezaji wote kwa pamona tutafanikisha hilo na kuendelea kywapa furaha mashabiki wetu,” amesema Guede ameongeza kuwa;

Yanga ina wachezaji wazuri sana japo bado sijawaon wote kwa sababu wengine wako kwenye majukumu ya timu za Taifa kwenye mashindano ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), naamini baada ya muda nitawafahamu wpte.

Kuhusu Pacome Zouzoua, Attohoula Yao na Aziz Ki ambao amewahi kuwa nao, amesema akiwa nao tayari anajihisi kuwa yuko nyumbani na hafikirii kupata shinda kwa sababu alipata nafasi ya kuzungumza nao kabla ya kuja nchini na wamemuambia ajihisi yuko nyumbani.

Guede amesema namba 14 ya jezi aliyochangia ni pendwa na ina bahati kwake kwa tangu klabu yake ya kwanza alikuwa anaivaa hiyo na kuipenda kwa sababu ya mchezaji wa zamani wa Barcelona na Monaco na sasa ni kocha wa timu ya vijana ya U 21 nchini Ufaransa.

SOMA NA HII  HIZI HAPA MBINU ZA KIJESHI ZA BENCHIKHA ZILIVYOWAMALIZA WYDAD LEO...GAME ILIISHIA HAPA...