Home Uncategorized KUMUONA BERNARD MORRISON NI BUKU TANO TU

KUMUONA BERNARD MORRISON NI BUKU TANO TU


LEO saa moja kamili Usiku, Uwanja wa Taifa kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Namungo FC. 

Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael mkali wao wa kucheka na nyavu ni David Molinga akiwa na mabao nane huku kwa Namungo mtupiaji wao namba moja ni Relliants Lusajo mwenye mabao 12.

Kuwaona nyota wa Yanga wakimenyana na Namungo, ikiwa ni pamoja na Bernard Morrison mwenye mabao matatu huku kwa Namungo akiwa ni Lukas Kikoti mwenye mabao manne kiingilio cha chini kabisa ni buku tano (5,000) kwa viti vya mzunguko.

 VIP A 15,000 , B&C 10,000 na mzunguko 5,000 huku kwa yule atakayenunua jezi ya Yanga kwa shilingi 20,000 atapewa tiketi bure ya mzunguko na jarida pia.


SOMA NA HII  ZLATAN IBRAHIMOVIC AWINDWA NA MABOSI WA SWEDEN