Home Uncategorized ZLATAN IBRAHIMOVIC AWINDWA NA MABOSI WA SWEDEN

ZLATAN IBRAHIMOVIC AWINDWA NA MABOSI WA SWEDEN

ZLATAN Ibrahimovic staa anayekipiga ndani ya Klabu ya AC Milan amewekwa kwenye rada na Klabu ya Hammarby ya nchini Sweden ambayo inataka kumpata akimalizana na timu yake ya sasa.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu ya Hammaby amesema mpango wao ni kupata saini ya nyota huyo pindi akimalizana na AC Milan.

Mkataba wa Zlatan na mabosi wake wa AC Milan unameguka mwishoni mwa msimu huu kwani alisaini kandarasi ya miezi sita pekee jambo linalowapa matumaini mabosi hao kumpata.

Zlatan raia wa Sweden amecheza mechi 10 na kutupia mabao manne aliwahi kukipiga ndani ya Barcelona,  Manchester United,  Ajax, PSG na LA Galaxy.

SOMA NA HII  PHIRI KAMA UTANI ILA NDO ANAKUJA IVO