Home Uncategorized YANGA YA GSM YAJITOSA UPYA KWA MAKAMBO WA HOROYA

YANGA YA GSM YAJITOSA UPYA KWA MAKAMBO WA HOROYA

YANGA wameamua kujilipua tena kwa straika wao wa zamani, Heritier Makambo anayekipiga AC Horoya ya Guinea.

Awali, Horoya waligoma kumuachia Mkongomani huyo kwa madai kwamba, wanamtegemea na ishu za yeye kukaa benchi haimaanishi kuwa hahitajiki kikosini.

Mwanaspoti limejiridhisha kwamba, Yanga wiki hii wametuma ofa ya mwisho kwa Makambo na wame kuwa wakizun gumza kiaina na staa huyo wa kuwajaza.

Habari zinasema kwamba wadhamini wao GSM ndio wametuma ofa hiyo ya pili mezani kwa Rais na Bilionea wa klabu hiyo Mamadou Antonio Souare.

Mmoja wa viongozi wa Yanga alisema jana kwamba, Antonio amewaambia anawafikiria atawajibu.

Katika barua hiyo ya Yanga ambayo Mwanaspoti iliiona, vijana hao wa Jangwani wamewaomba Horoya kutoa ushirikiano wao kwa lengo la kuokoa kipaji chake kutokana na kushindwa kuingia katika kikosi cha kwanza.

Yanga wamewaambia Horoya kwamba, wako tayari hata kumpokea kwa mkopo.

“Ngoja tusubiri watatuletea jibu gani bado tuna muda na kwa kuwa wao wametuambia watatujibu wiki ijayo tutasubiri tuone wataamua nini,” alieleza mmoja wa mabosi wa Yanga.

Utata mkubwa wa kuamua hatma hiyo utabaki wa Soure, ambaye ni shabiki mkubwa wa Makambo aliyemnunua kwa Euro 70,000 (Sh176 milioni) kutoka Jangwani.

Hatua nyingine ni mkataba wa Makambo na Horoya ambao umebakiza miaka mitatu ambapo, klabu hiyo haitakuwa katika presha yoyote ya kufanya maamuzi ya kufanya biashara na Yanga.

GSM nao hawataki kitumia fedha nyingi katika kumsajili Makambo, ambaye alifunga mabao 17 kabla ya kuuzwa akiwa Mfungaji Bora ndani ya kikosi hicho, wakisema wana machaguo bora ukiondoa Makambo.

“Hata upande wa pili (Simba) tunajua kwamba kila wanaposikia Makambo anarudi kisha aje acheze na Morrison (Bernard) pamoja na Haruna (Niyonzima) wanapata presha huko.

“Hivyo hatutaki kutumia fedha nyingi kwa Makambo kwa kuwa wapo washambuliajiwachezaji wengine ambao wataunda safu bora ya ushambuliaji hata kama tutamkosa Makambo. Jambo la msingi mwenyewe (Makambo) anahitaji kurudi Jangwani ana anatupa ushirikiano mkubwa katika hili,” alisema bosi huyo.

SOMA NA HII  CORONA IMEFUTA LIGI ZA NCHI HIZI HAPA MSIMU WA 2019/20