Home news WAKATI WATU WAKIFIRI NI ‘NDUMBA’ ZA MAYELE….NABI AANIKA SIRI YA KUPENDA KUMTUMIA…

WAKATI WATU WAKIFIRI NI ‘NDUMBA’ ZA MAYELE….NABI AANIKA SIRI YA KUPENDA KUMTUMIA…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ametaja mambo muhimu ya Fiston Mayele yanayofanya aweze kuanza moja kwa moja kikosi cha kwanza.

Mayele ni mtupiaji namba moja ndani ya Yanga akiwa ametupia mabao 10 na pasi tatu katika mechi 17 ambazo Yanga imecheza ikiwa na pointi 45 kibindoni.

Nabi alisema kuwa Mayele ana mambo mengi ya muhimu ambayo anayafanya kabla ya mechi na kwenye mechi ikiwa ni pamoja na nidhamu pamoja na juhudi katika mazoezi.

β€œMayele ni mchezaji mzuri unaona kwamba anaanza kikosi cha kwanza kwenye mechi nyingi kwa sababu ana nidhamu pia amekuwa akitoa ushirikiano kwa wachezaji pamoja na juhudi mazoezini na hata kwenye mechi pia.

β€œAkianza kwenye mechi amekuwa akiweza kufunga na wakati mwingine amekuwa akitoa pasi za mabao hivi ni vitu alivyonavyo na kila mchezaji ni muhimu kwenye kikosi hilo kila mmoja analitambua,” alisema Nabi.

Mchezo ujao wa Yanga ni dhidi ya KMC timu ambayo ilikuwa ya kwanza kufungwa na Mayele mchezo uliochezwa Uwanja wa Majimaji, Songea.

SOMA NA HII  HUO MKATABA MPYA WA SIMBA NA MANULA HAKUNA TZ NZIMA...SASA NDIYE MCHEZAJI GHALI KULIKO WOTE NCHINI...