Home CAF AL AHLY WAICHAPA AS VITA KWAO, KUNDI A NI NOMA

AL AHLY WAICHAPA AS VITA KWAO, KUNDI A NI NOMA

 


KLABU ya Al Ahly ya Misri leo Machi 16 imesepa na pointi tatu muhimu ikiwa ugenini kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika,  hatua ya makundi.

Uwanja wa Des Martyrs ubao ulisoma AS Vita 0-3 Al Ahly ambapo mabao yalianza kupachikwa kupitia kwa Mohamed Sherif dakika ya 6.

Dakika ya 19 Mohamed Magdy yeye alipachika bao la pili dakika ya 19 na kufanya waende mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0.

Ni Taher Mohamed alipachika bao la tatu na la mwisho dakika ya 78.

Kundi A kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika limekuwa na ushindani mkubwa ambapo kinara ni Simba mwenye pointi 10 huku Al Ahly akiwa na pointi 7 nafasi ya pili.

Al Merrikh ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi moja na AS Vita ipo nafasi ya tatu na ina pointi 4.



SOMA NA HII  YANGA WAMEAMUA, CHEKI NDEGE WATAKAYOPANDA KUWAFUATA RIVERS UNITED, NIGERIA