Home Habari za michezo MANGUNGU TUPA DONGO JANWANI, KUHUSU SIMBA DAY, NA WIKI YA WANANCHI, MAMBO...

MANGUNGU TUPA DONGO JANWANI, KUHUSU SIMBA DAY, NA WIKI YA WANANCHI, MAMBO YAPAMBA MOTO

mangungu

Heee!! Mmesikia huko? Eti kuna timu imeiga tamasha la Simba Day? Mbona Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu amesema kuwa watu wameiga kwao wakatoa neno ‘Day’ wakaweka ‘Wiki’.

Sawa hebu tuchambue hapa! Ukiachana na Simba SC, timu zinazofanya matamasha ya aina hii ni Yanga SC na Singida Fountain Gate, la Singida linatiwa ‘Singida Big Day’ neno ‘Day’ halijaondolewa hapo, tamasha la Yanga linaitwa Wiki ya Wananchi sasa ni wazi kuwa Mangungu ameikusudia Yanga kuwa ndio wameiga maana ndio wanaotumia neno ‘Wiki’

Lakini wanasemaga kitu kizuri kinaigwa, kuna shida kwani Yanga kuiga kizuri kutoka kwa watani wao? Kwani sio hawa wakikaa vijiweni wanasema ni wa baba mmoja na wengine wanasema mmoja katokea ubavuni kwa mwenzie.

Labda pengine tabu ya hizi timu mbili huwa hazitaki kuonekana mmoja yuko chini ya mwenzie au hawapendi kujishusha na shida huanzia hapo, sawa basi tuiache kama ilivyo.
Niambie wewe ni kweli Yanga imeiga kutoka kwa Simba?

SOMA NA HII  SABABU ZA KAPOMBE NA ZIMBWE KUTEMWA...KAPOMBE HANA SPIDI...ZIMBWE JR HANA UMAKINI